HABARI KUBWA LEO,DK SLAA AMWAGA MANYANGA RASMI,AACHA SIMANZI UKAWA,SOMA HAPO KUJUA
KATIBU mkuu wa CHADEMA Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema aliamua kuachana na CHADEMA na siasa kwa ujumla tangu tarehe 28/08/2015 baada ya Mbunge wa Monduli Edward Lowasa kujiunga na CHADEMA, kwa kile alicho dai kuwa asingeweza kushiriki kumsafisha mtu mwenye madhambi na badala yake aliona ni vyema ajiengue kwakuwa yeye sio muumini wa siasa za ulaghai.
Kauli hiyo ameitoa katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, amabapo amesema ameamua kayasema hadharani kwa kile alicho dai kuna upotoshwaji unao endelea kuwa yuko likizo na kwamba atajiunga na shughuli za chama hicho mbele ya safari, huku akidai kuwa hakuwa likizo na wala hakupewa barua yoyote ya likizo
Hata hivyo amesema alijaribu mara kadhaa kuandika baraua za kujiuzuru lakini hakuweza kusikilizwa na mtu yoyote, na baadae aliamua kuchukua uamuzi wa kuchana shughuli za chama hicho, na kwamba uvumi uliokuwa ukiendelea kuwa Slaa amezuiwa na mke wake Josephine
No comments :
Post a Comment